Hud 11:31
هودوَلَآ أَقُولُ لَكُمْ عِندِى خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعْلَمُ ٱلْغَيْبَ وَلَآ أَقُولُ إِنِّى مَلَكٌ وَلَآ أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِىٓ أَعْيُنُكُمْ لَن يُؤْتِيَهُمُ ٱللَّهُ خَيْرًا ۖ ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا فِىٓ أَنفُسِهِمْ ۖ إِنِّىٓ إِذًا لَّمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Wala siwaambii kuwa nina hazina za Mwenyezi Mungu, wala kuwa mimi ninajua mambo ya ghaibu, wala sisemi: Mimi ni Malaika. Wala sisemi kuhusu wale ambao yanawadharau macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa heri. Mwenyezi Mungu ndiye anayajua zaidi yaliyo katika nafsi zao. Hapo bila ya shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala sikwambiini kuwa nina khazina za Mwenyezi Mungu; wala kuwa mimi najua mambo ya ghaibu; wala sisemi: Mimi ni Malaika. Wala siwasemi wale ambao yanawadharau macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa kheri - Mwenyezi Mungu anajua yaliomo katika nafsi zao - hapo bila ya shaka ninge kuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. [31]
[31] Wala sikwambiini kuwa kwa sababu mimi ni Mtume, basi ninazo khazina za riziki ya Mwenyezi Mungu, nitumie nitakavyo, na kwa hivyo nimfanye anaye nifuata tajiri! Wala sikwambiini kuwa mimi najua mambo ya ghaibu, na kwa hivyo nikupeni khabari yale yaliyo mkhusu Mwenyezi Mungu tu kuyajua, kwa kuwa hapana mja yeyote anaye yajua! Wala mimi sikwambiini kuwa mimi ni Malaika, na kwa hivyo mnirudi kwa kauli yenu: Huyu si chochote ila mwanaadamu tu! Wala siwasemi wale mnao wadharau kwamba Mwenyezi Mungu hatowapa kheri yoyote kwa kutaka kuridhi myatakayo! Kwani Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anaye jua ikhlasi iliomo katika nafsi zao!..Mimi nikisema myatakayo nitakuwa katika wenye kujidhulumu na kudhulumu wengineo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Na wala siwaambii nyinyi kuwa mimi nina mahazina ya Allah Mtukufu, na mimi siyajui yasiyoonekana, na mimi si mmoja kati ya Malaika, wala siwaambii hawa mnaowadharau miongoni mwa madhaifu wa Waumini kwamba Allah Mtukufu hatawapa malipo mema ya matendo yao. Allah Mtukufu, Peke Yake, ni Mjuzi kabisa kwa yaliyomo ndani ya vifua vyao na nyoyo zao. Na nikifanya hivyo, basi mimi wakati huo nitakuwa ni miongoni mwa wale wenye kujidhulumu wao wenyewe na kuwadhulumu wengineo»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net