Hud 11:24
هودمَثَلُ ٱلْفَرِيقَيْنِ كَٱلْأَعْمَىٰ وَٱلْأَصَمِّ وَٱلْبَصِيرِ وَٱلسَّمِيعِ ۚ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Mfano wa makundi mawili haya ni kama kipofu na kiziwi, na mwenye kuona na anayesikia. Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamkumbuki?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu kiziwi, na mwenye kuona na anasikia. Je, wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamfikiri? [24]
[24] Mfano wa makundi mawili hayo, ya Waumini na makafiri, ni kama kipofu anaye kwenda bila ya uwongofu na kiziwi asiye sikia uwongozi wa kuokoka, na kundi la pili ni kama mwenye macho anaye iona njia ya kheri na uokofu, na mwenye masikio makali anaye sikia kila lenye manufaa naye. Makundi mawili hayo hayawezi kuwa sawa katika hali yao na kuishia kwao! Basi, enyi watu, hamfikiri yaliyo baina yenu ya khitilafu ya utambuzi na ukafiri, na khitilafu baina ya baat'ili na Haki, mkawa mbali na njia ya upotovu, na mkaishika Njia Iliyo Nyooka?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mfano wa makundi mawili, ya ukafiri na Imani, ni mfano wa kipofu asiyeona na kiziwi asiyesikia na yule anayeona na kusikia: kundi la ukafiri haliioni haki likapata kuifuata wala halimsikii mlinganizi wa Allah Mtukufu likapata kuongoka kwa sababu yake. Ama kundi la Imani limeshaziona hoja za Allah Mtukufu na limemsikia mlinganizi wa Allah Mtukufu na limemuitikia. Je, yanafanana makundi mawili haya? Kwani hamzingatii na mkafikiri?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net