Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 23

Hud 11:23

هود

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَأَخْبَتُوٓا۟ إِلَىٰ رَبِّهِمْ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Hakika, wale walioamini, na wakatenda mema, na wakanyenyekea kwa Mola wao Mlezi, hao ndio watu wa Bustanini, humo watadumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walio amini,na wakatenda mema, na wakanyenyekea kwa Mola wao Mlezi, hao ndio watu wa Peponi, na humo watadumu. [23]

[23] Bila ya shaka wale wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wakatenda a'mali njema, na nyoyo zao zikanyenyekea na zikatua kuikubali hukumu ya Mola wao Mlezi, hao ndio wanao stahiki kuingia Peponi na kudumu humo milele.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale ambao walimuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema, wakanyenyekea kwa Allah Mtukufu katika kila walichoamrishwa na kukatazwa. Hao ndio watu wa Peponi, hawatakufa humo wala hawatatoka kabisa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net