Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 22

Hud 11:22

هود

لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ هُمُ ٱلْأَخْسَرُونَ

Maana

Hakuna shaka kwamba wao katika Akhera ndio waliohasiri zaidi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Bila ya shaka hakika wao ndio wenye kukhasiri huko Akhera. [22]

[22] Kweli, hakika wao Siku ya Akhera ndio wenye kukhasiri kuliko watu wote!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ukweli ni kwamba wao kesho Akhera ni wenye kupata hasara zaidi kibiashara, kwa kuwa wao waliacha daraja za Pepo na kuchukuwa mashimo ya Moto, kwa hivyo wakawa kwenye Moto wa Jahanamu. Huko ndiko kupata hasara waziwazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net