Hud 11:21
هودأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ
Hao ndio waliozihasiri nafsi zao, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyazua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio walio zikhasiri nafsi zao, na yakawapotea waliyo kuwa wakiyazua. [21]
[21] Hao makafiri hawapati faida yoyote katika kumuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu! Bali wamejikhasiri nafsi zao, na huko Akhera huo uwongo walio kuwa wakiuzua, na madai ya upotovu, na miungu ya uwongo waliyo kuwa wakiiunda, na wakadai kuwa hiyo ati ikiwafaa au itawaombea - yote hayo yatawapotea. Kwa sababu hakika Siku ya Kiyama ndiyo Siku ya hakika, ambayo haina udanganyifu wala uzushi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao ndio wale waliopata hasara ya nafsi zao kwa kumzulia kwao Allah Mtukufu urongo na waliwaondokea wao waungu waliokuwa wakiwazua na kudai kwamba wao watawaombea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net