Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 20

Hud 11:20

هود

أُو۟لَـٰٓئِكَ لَمْ يَكُونُوا۟ مُعْجِزِينَ فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنْ أَوْلِيَآءَ ۘ يُضَـٰعَفُ لَهُمُ ٱلْعَذَابُ ۚ مَا كَانُوا۟ يَسْتَطِيعُونَ ٱلسَّمْعَ وَمَا كَانُوا۟ يُبْصِرُونَ

Maana

Hao hawakuwa ni wa kushinda katika ardhi, wala hawana walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu. Watazidishiwa adhabu; kwa kuwa, hawakuwa wakiweza kusikia wala hawakuwa wakiona.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao hawawezi kushinda katika ardhi, wala hawana walinzi isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Watazidishiwa adhabu. Hawakuwa wakiweza kusikia wala hawakuwa wakiona. [20]

[20] Hao makafiri hawana nguvu za kumshinda Mwenyezi Mungu asiwatie nguvuni duniani akawaadhibu; na hawana wasaidizi wa kuweza kuwakinga na adhabu yake pindi Mwenyezi Mungu akitaka kuwaletea hiyo katika Akhera, hata ikiwa mardufu ya ile ambayo wangeli ipata duniani, ingeli kuwa Mwenyezi Mungu anataka iwafikie. Kwa sababu hao wamechukia kuisikia Qur'ani, na kuzingatia Ishara za Mwenyezi Mungu katika ulimwengu. Wamekuwa kama kwamba hawakuwa wakiweza kusikia wala kuona.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Makafiri hao hawakuwa ni wenye kumkwepa Allah Mtukufu kwa kumkimbia, na hawakuwa na wasaidizi wa kuwazuia wao wasipate mateso ya Allah Mtukufu. Wataongezewa adhabu katika Jahanamu, kwa kuwa wao walikuwa hawawezi kuisikia Qur’ani kwa namna ya kuwafanya wanufaike au wazione alama za Allah Mtukufu katika ulimwengu kwa namna ya kuwafanya waongoke, kwani wao walikuwa wameshughulika na ukafiri ambao walikuwa wamedumu nao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net