Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 19

Hud 11:19

هود

ٱلَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ كَـٰفِرُونَ

Maana

Ambao wanazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaitakia ijipinde, nao wanakufuru Akhera.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ambao wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaitakia ipotoke, na wanaikataa Akhera. [19]

[19] Hawa ndio wanawageuza watu wasiifuate Dini ya Mwenyezi Mungu, na wanawazuia. Nayo hiyo ndiyo Njia yake Iliyo Nyooka. Na wanataka Njia hii iwafikiane na matamanio yao na pumbao lao, kwa hivyo yende upogo. Hao wanaikanya Akhera, na yaliyomo ndani ya kulipwa thawabu Muumini na kuadhibiwa kafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawa madhalimu ni wale ambao wanawazuia watu na njia ya Allah Mtukufu yenye kupelekea kumuabudu na wanataka njia hii iwe imepinda ili iambatane na matamanio yao na wao wanaikanusha Akhera, hawaamini kufufuliwa wala kulipwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net