Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 18

Hud 11:18

هود

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ ٱلْأَشْهَـٰدُ هَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo? Hao wataletwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema, "Hawa ndio waliomdanganyishia Mola wao Mlezi. Sikilizeni! Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate madhalimu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na nani aliye dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Hao watahudhurishwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema: Hawa ndio walio mtungia uwongo Mola wao Mlezi. Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu, [18]

[18] Hapana walio zidi kujidhulumu nafsi zao na wakajitenga mbali na Haki kuliko wale wanao tunga uwongo, na kisha wakamnasibishia Mwenyezi Mungu. Hakika watu hawa Siku ya Kiyama watadhihirishwa mbele ya Mola wao Mlezi awahisabie kwa yale maovu waliyo yatenda. Mashahidi miongoni mwa Malaika, na Manabii, na wengineo, watasema: Hawa ndio walio tenda makosa maovu kabisa na dhulma kwa mintarafu ya Muumba wao! Hapana shaka laana ya Mwenyezi Mungu itawapata hao kwa kuwa ni wenye kudhulumu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hakuna yoyote aliye dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah Mtukufu urongo. Hao watahudhurishwa kwa Mola wao Siku ya Kiyama, ili Awahesabu kwa matendo yao. Na watasema waliohudhuria miongoni mwa Malaika na Manabii na wengineo, «Hawa ndio wale waliosema urongo kumsingizia Mola wao ulimwenguni. Allah Mtukufu Amewakasirikia wao na Amewalaani laana isiyokatika, kwa kuwa udhalimu walioufanya umekuwa ni sifa inayoambatana na wao».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net