Hud 11:25
هودوَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِۦٓ إِنِّى لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
Na hakika, tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akawaambia, "Hakika mimi ni mwonyaji aliye wazi kwenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akawaambia: Hakika mimi ni mwonyaji kwenu ninaye bainisha, [25]
[25] Na kama tulivyo kutuma kwa watu wako uwaonye na uwabashirie kheri, wakakukabili baadhi yao kwa inadi na upinzani, kadhaalika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akawaambia: Mimi nakuhadharisheni na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na nakuonyesheni njia ya kuokoka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika tulimtuma Nûh, kwa watu wake akasema kuwaambia, Mimi ni muonyaji kwenu adhabu ya Allah Mtukufu, ni mwenye kuwabainishia yale niliyotumwa kwenu ya maamrisho ya Allah Mtukufu na makatazo yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net