Hud 11:13
هودأَمْ يَقُولُونَ ٱفْتَرَىٰهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا۟ بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِۦ مُفْتَرَيَـٰتٍ وَٱدْعُوا۟ مَنِ ٱسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Au wanasema, "Ameizua?" Sema, "Basi leteni sura kumi zilizozuliwa mfano wake, na waiteni muwawezao isipokuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura kumi zilizo zuliwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli. [13]
[13] Katika Qur'ani ipo Ishara inayo thibitisha ukweli wako. Basi wao wakisema, kuwa hii umeitunga wewe na umemzulia Mwenyezi Mungu, wewe waambie: Ikiwa Qur'ani hii imetokana na mwanaadamu, basi yamkinika mwanaadamu mwengine kuleta mfano wake. Na nyinyi ni mafasihi kuliko wote. Basi leteni Sura kumi kama hii mbali mbali, na mtakeni msaada yeyote mnaye weza kumtaka, katika watu na majini, kama hakika mnasema kweli katika hayo madai yenu kuwa haya ni maneno ya binaadamu. Qur'ani si muujiza tu katika maandishi yake, bali ndani yake mna hadithi za kweli, na ilimu mbali mbali za sayansi za uumbaji zilizo ashiriwa, na hazikuwa zikijuulikana wakati wa kuteremka kwake, na pia katika hukumu ziliomo ndani yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au je, washirikina hawa, miongoni mwa watu wa Makkah, wanasema kwamba Muhammad ameizua hii Qur’ani? Waambie basi, «Iwapo mambo ni kama mnavyodai, leteni sura kumi mfano wake za kuzuliwa, na muwaite mnaowaweza miongoni mwa viumbe wote wa Allah Mtukufu, ili wawasaidie kuzileta hizi sura kumi, iwapo nyinyi ni wa kweli katika madai yenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net