Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 12

Hud 11:12

هود

فَلَعَلَّكَ تَارِكٌۢ بَعْضَ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيْكَ وَضَآئِقٌۢ بِهِۦ صَدْرُكَ أَن يَقُولُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَآءَ مَعَهُۥ مَلَكٌ ۚ إِنَّمَآ أَنتَ نَذِيرٌ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ وَكِيلٌ

Maana

Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyofunuliwa kwako, na kifua chako kikaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema, "Mbona hakuteremshiwa hazina, au Malaika akaja pamoja naye?" Hakika, wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyo funuliwa kwako, na kifua kitaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema: Mbona hakuteremshiwa khazina, au wakaja naye Malaika? Wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa kila kitu. [12]

[12] Ewe Nabii! Usijaribu kutaka kuwaridhi washirikina, kwani hao hawaamini. Na huenda ukijaribu kutaka kuwaridhi ukaacha kusoma baadhi ya uliyo letewa Wahyi, katika yale wasiyo penda wao kuyasikia, kama vile kudharauliwa baadhi ya miungu yao, kwa kukhofu kuwa wasije wakakejeli! Na huenda pengine ukahisi dhiki unapo wasomea, kwa kuwa wao wanataka Mwenyezi Mungu akuteremshie khazina ustarehe nayo kama wafalme, au waje nawe malaika watwambie ukweli wake! Basi, ewe Nabii! Usizibali inadi zao. Kwani wewe si chochote ila ni mwonyaji na mhadharishaji wa adhabu za Mwenyezi Mungu kwa anaye kwenda kinyume na amri yake. Nawe hayo umefanya, basi jipumzishe nafsi yako nao. Na jua kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuangalia na kulinda kila kitu. Naye atawafanyia kama wanavyo stahiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Huenda wewe, ewe Mtume, kwa ukafiri na ukanushaji mkubwa unaouona kwao, ukawa ni mwenye kuyaacha baaadhi ya yale unayoletewa wahyi kati ya yale ambayo Allah Mtukufu Alikuteremshia na Akakuamuru kuyafikisha, na kifua chako kikawa ni chenye kuhisi dhiki kwa hayo, kwa kuogopa wasije wakataka baadhi ya mambo kutoka kwako kwa njia ya kukusumbua, kama vile kusema, «Kwa nini asiteremshiwe mali mengi, au asijiwe na Malaika ambaye atamuamini katika ujumbe wake?» Basi wafikishie yale niliyokuletea wahyi kwayo, kwani lako wewe si lingine isipokuwa ni kuonya kwa yale uliyoletewa wahyi. Na Allah Mtukufu ni Mtunzi wa kila kitu, Anaendesha mambo yote ya viumbe vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net