Hud 11:14
هودفَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَكُمْ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَآ أُنزِلَ بِعِلْمِ ٱللَّهِ وَأَن لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ
Na wasipokuitikieni, basi jueni ya kwamba (hii Qur-ani) imeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye. Basi je, nyinyi ni Waislamu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wasipo kuitikieni, basi jueni ya kwamba (hii Qur'ani) imeteremshwa kwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hapana mungu ila Yeye. Basi je! Nyinyi ni Waislamu? [14]
[14] Mkishindwa, na wakashindwa mlio wataka msaada, kuleta mfano wake hii wa kuzua, basi jueni kuwa Qur'ani haikuteremshwa ila kwa kuambatana na ujuzi wake Mwenyezi Mungu. Ilimu yake haijui mtu ila Yeye. Na jueni kuwa hapana mungu ila Allah, Mwenyezi Mungu tu. Hapana anaye tenda kazi yake. Basi kuweni Waislamu baada ya kwisha thibiti hoja hizi juu yenu, kama nyinyi mnataka Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Iwapo washirikina hawa hawatawaitikia nyinyi, ewe Mtume na walio pamoja na wewe, kwa yale mnayowaitia, kwa kulemewa kufanya hivyo, basi jueni kwamba hii Qur’ani, kwa hakika Allah Mtukufu Amemteremshia Mtume Wake kwa ujuzi Wake, na si maneno ya binadamu. Na jueni kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Mtukufu. Je nyinyi, baada ya kusimama hoja hii kwenu, ni wenye kujisalimisha, ni wenye kunyosha shingo kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net