Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 120

Hud 11:120

هود

وَكُلًّا نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنۢبَآءِ ٱلرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِۦ فُؤَادَكَ ۚ وَجَآءَكَ فِى هَـٰذِهِ ٱلْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Na yote tunayokusimulia katika habari za Mitume yale tunayoimarisha kwayo (ufahamu wa) moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na yote tunayo kusimulia katika khabari za Mitume ni ya kukupa nguvu moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini. [120]

[120] Ewe Nabii! Tunakusimulia kila namna ya khabari ya Mitume walio pita pamoja na kaumu zao kwa ajili ya kukupa nguvu wewe uweze kubeba mashaka ya Utume. Na katika khabari hizi yamekujia maelezo ya haki unayo ilingania mfano walivyo lingania Mitume walio kutangulia, nayo ni Tawhidi ya kuwa Mwenyezi Mungu ni Mpweke, na kuepuka yale ambayo yanamkasirisha, kama yalivyo wajia mawaidha na mazingatio yanayo wanufaisha Waumini, ili wazidi imani yao, na wanao jitayarisha kwa imani ili waifanyie haraka hiyo imani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tunakupa habari, ewe Mtume, za Mitume waliokuwa kabla yako zenye kila unalohitajia la kuupa nguvu moyo wako ya kusimama imara ili kubeba majukumu ya Utume. Na umekujia wewe, katika sura hii na habari zilizomo, ufafanuzi wa haki ambayo wewe uko juu yake. Na yamekujia wewe, katika hii sura, mawaidha ya kuwafanya makafiri wakomeke na ukumbusho wa kuwafanya wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake wakumbuke.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net