Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 121

Hud 11:121

هود

وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ٱعْمَلُوا۟ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنَّا عَـٰمِلُونَ

Maana

Na waambie wale wasioamini, "Fanyieni mahali penu, nasi hakika pia tunafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na waambie wale wasio amini: Fanyeni muwezavyo, nasi pia tunafanya. [121]

[121] Ewe Nabii! Waambie hao wanao shikilia inadi na ukafiri: Tendeni kama mnavyo weza kuupiga vita Uislamu na kuwaudhi Waumini. Sisi tunaendelea na njia yetu, na tumethibiti katika a'mali yetu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Mtume, makafiri wasiokubali upweke wa Allah Mtukufu, «Fanyeni mnayoyafanya kwa namna yenu na mbinu zenu za kuupinga Ulinganizi na kumkera Mtume na wale waliomuitika, kwani sisi ni wenye kufanya kwa namna yetu mbinu zetu za kusimama imara juu ya Dini yetu na kutekeleza amri ya Allah Mtukufu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net