Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 119

Hud 11:119

هود

إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلْجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجْمَعِينَ

Maana

Isipokuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu. Na kwa hiyo ndiyo Mwenyezi Mungu amewaumba. Na lilitimia neno la Mola wako Mlezi kwamba hakika nitaijaza Jahannam kwa majini na watu kwa pamoja.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba. Na litatimia neno la Mola wako Mlezi: Kweli kweli nitaijaza Jahannam kwa majini na watu pamoja. [119]

[119] Lakini wale Mwenyezi Mungu alio warehemu kwa kusalimika kwao kwa walivyo jaaliwa, hao wameridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu juu yao, wakawaamini Mitume wake wote, na Vitabu vyake vyote, na Siku ya Mwisho. Na kwa namna hivi ilivyo pita hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mpango wa huu ulimwengu ndivyo alivyo waumbia Subhanahu kwa kuwaweka tayari kuwateua na kuwavusha na hizo khitilafu, ili aweke tayari panapo stahiki thawabu na adhabu. Kwa hivyo ahadi ya Mola wako Mlezi itatimia ya kwamba hapana budi kuwa ataijaza Jahannamu kwa wafuasi wa Iblis miongoni mwa majini na watu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Isipokuwa wale waliorehemewa na Mola wako, wakamuamini Yeye na wakawafuata Mitume Wake, kwani wao hawatafautiani juu ya kumpwekesha Allah Mtukufu na yale ambayo Mitume wamekuja nayo kutoka kwa Allah Mtukufu. Ni matakwa ya Hekima Yake, Aliyetakasika na sifa za upungufu na Akatukuka, kwamba Yeye Amewaumba wao wakiwa wametafautiana: kuna kundi ovu na kundi lema; na kila kundi limesahilishiwa kwa lile lililoumbiwa, na kwa hii ndipo agizo la Allah Mtukufu litatimia la kuwa Yeye Ataujaza, Moto wa Jahanamu, majini na binadamu waliomfuata Iblisi na askari wake na wasiongoke kwenye njia ya Imani.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net