Hud 11:118
هودوَلَوْ شَآءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ ٱلنَّاسَ أُمَّةً وَٰحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ
Na Mola wako Mlezi angelitaka, angewafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kuhitilafiana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana,. [118]
[118] Ewe Nabii! Lau kuwa Mola wako Mlezi angeli penda angeli wafanya watu wote wafuate Dini moja, wakimt'ii Mwenyezi Mungu kwa ut'iifu wa maumbile, kama Malaika. Na ulimwengu ungeli kuwa sio ulimwengu huu. Lakini Yeye Subhanahu hakutaka hayo, bali amewaacha waweze kuchagua wenyewe. Basi hawaachi kukhitalifiana katika kila kitu, hata katika misingi ya imani, kama kumuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho - mambo ambayo haifai kukhitalifiana kwayo. Wao hufuata nyoyo zao, na matamanio yao, na fikra zao, kila kikundi kimeshikilia kwa nguvu rai ile ile walio kutana nayo kwa baba zao!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau Mola wako angetaka, Angaliwafanya watu wote ni kundi moja, wako kwenye dini moja, nayo ni dini ya Uislamu. Lakini Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, hakutaka hivyo. Basi watu hawataacha kuendelea kutafautiana katika dini zao, na hayo ndiyo yanayoambatana na hekima Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net