Hud 11:117
هودوَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ ٱلْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ
Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuiangamiza miji kwa dhuluma tu ilhali watu wake ni watenda mema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema. [117]
[117] Wala sio mwendo wake Mwenyezi Mungu, wala sio uadilifu wake wa maumbile, kuudhulumu umma wowote akauteketeza nao unashikamana na Haki, unafuata mwendo bora, unatenda yanao wafaa wao na wenginewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakuwa Mola wako, ewe Mtume, ni Mwenye kuuangamiza mji wowote miongoni mwa miji na hali watu wake ni wenye kufanya mambo mazuri katika ardhi, wenye kujiepusha na uharibifu na udhalimu; Yeye huwaangamiza wao kwa sababu ya udhalimu wao na uharibifu wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net