Hud 11:116
هودفَلَوْلَا كَانَ مِنَ ٱلْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُو۟لُوا۟ بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْفَسَادِ فِى ٱلْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ ۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مَآ أُتْرِفُوا۟ فِيهِ وَكَانُوا۟ مُجْرِمِينَ
Basi mbona hawakuwepo katika vizazi vya kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanaokataza uharibifu katika nchi, isipokuwa wachache tu, miongoni mwa wale tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu walifuata yale waliyostareheshwa kwayo, na walikuwa wahalifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao, na wakawa ni wakosefu. [116]
[116] Ilikuwa inapasa katika kaumu zilizo tangulia na tukaziteketeza kwa dhulma zao, wawepo jamaa kati yao wenye kusikilizwa kauli yao, na wenye vyeo katika dini na akili, wawakanye wenzi wao waache uharibifu katika nchi, ili wasalimike na adhabu iliyo wateremkia. Lakini hayakuwa hayo. Yaliyo tokea ni kuwa walikuwapo Waumini wachache wasio sikilizwa rai zao wala uwongozi wao. Hao Mwenyezi Mungu aliwaokoa pamoja na Mitume wao wakati ule walipo shikilia wenye kudhulumu wenye inda kung'ang'anilia yale maisha ya anasa na fisadi waliyo yazoea. Hayo yakawa ni pingamizi wasiweze kunafiika na wito wa Haki na kheri, na kwa kukhiari kwao njia hiyo wakazama katika madhambi na vitendo viovu. Basi Mwenyezi Mungu akawahiliki kwa mujibu wa mwendo wake wa maumbile.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Laiti wangepatikana, miongoni mwa vizazi viliyopita kabla yenu, wasalia wa watu wazuri walio wema wanaowakataza makafiri waache ukafiri wao na kufanya uharibifu katika ardhi. Hawakupatikana katika hao isipokuwa wachache miongoni mwa walioamini na Allah Mtukufu akawaokoa na adhabu Yake Alipowapatiliza madhalimu. Na waliozidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wa kila ummah uliopita, walifuata ladha za duniani na anasa zake walizostareheshwa, na wakawa wahalifu, wenye kudhulumu kwa kufuata kwao starehe walizokuwa nazo, ndipo adhabu ikathibiti juu yao. Katika hii aya pana mazingatio na mawaidha kwa wanaofanya maasia miongoni mwa Waislamu, kwa kuwa hawaepukani na udhalimu wa nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net