Hud 11:115
هودوَٱصْبِرْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُحْسِنِينَ
Na subiri, kwani hakika Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wafanyao mazuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na subiri, kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wanao fanya wema. [115]
[115] Ewe Nabii! Vumilia mashaka ya haya tunayo kuamrisha, na yatimize vilivyo. Mwenyezi Mungu atakulipa malipo makubwa. Kwani kwake Yeye hayapotei malipo ya watendao mema kwa mujibu wa vitendo vyao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na usubiri, ewe Nabii, juu ya hiyo Swala na juu ya makero unayoyakuta kutoka kwa washirikina wa watu wako, kwani Allah Mtukufu Hapotezi malipo ya walio wema katika matendo yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net