Hud 11:114
هودوَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَىِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ ٱلَّيْلِ ۚ إِنَّ ٱلْحَسَنَـٰتِ يُذْهِبْنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّٰكِرِينَ
Na dumisha Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mazuri huondoa mabaya. Huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na shika Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanao kumbuka. [114]
[114] Ewe Nabii! Timiza Swala kwa ukamilifu katika ncha mbili za mchana, na nyakati mbali mbali za usiku. Kwani Swala husafisha nafsi na hushinda katika kung'oa shari, na hufuta athari ya maovu ambayo mwanaadamu shida kuepukana nayo! Hayo uliyo amrishwa, ewe Nabii, katika uwongofu wa kheri ni mawaidha ya kuwanufaisha wale ambao walio tayari kuyakubali, ambao kwamba wanamkumbuka Mola wao Mlezi, wala hawamsahau.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tekeleza Swala, ewe Nabii, kwa njia ya ukamilifu katika ncha mbili za mchana: asubuhi na jioni, na katika nyakati za usiku. Kwani kufanya mema kunafuta dhambi zilizopita na kuondoa athari zake. Kuamrisha kusimamisha Swala na kueleza kwamba mema huondoa mabaya ni mawaidha kwa anayewaidhika nayo na akakumbuka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net