Hud 11:113
هودوَلَا تَرْكَنُوٓا۟ إِلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ فَتَمَسَّكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنْ أَوْلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ
Wala msiwategemee wale waliodhulumu, mkaja kuguswa na Moto. Wala nyinyi hamna walinzi wowote kando na Mwenyezi Mungu, wala tena hamtanusuriwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa. [113]
[113] Wala msiwapende hata kidogo maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu walio zidhulumu nafsi zao na wakapindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu. Wala msiwategemee, au mkapendezewa na mwendo wao, na kwa kumili huko mkastahiki adhabu ya Moto, na msimpate yeyote wa kuwatetea. Mwisho wenu mtakuwa hamtanusuriwa kwa maadui zenu kwa kuwa Mwenyezi Mungu atakutupeni na kwa kuwa nyinyi mnamtegemea adui yake!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msilemee upande wa hawa makafiri walio madhalimu, msije mkapatwa na Moto. Na hamna nyinyi msaidizi mwenye kuwanusuru na kusimamia mambo yenu isipokuwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net