Hud 11:112
هودفَٱسْتَقِمْ كَمَآ أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا۟ ۚ إِنَّهُۥ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Basi, nyooka kama ulivyoamrishwa, wewe na wale wanaotubia kwa Mwenyezi Mungu pamoja nawe, wala msivuke mipaka. Hakika Yeye anayaona yote myatendayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi, simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa, wewe na wale wanao elekea kwa Mwenyezi Mungu pamoja nawe; wala msikiuke mipaka. Hakika Yeye anayaona yote myatendayo. [112]
[112] Ikiwa hii ndiyo hali ya kaumu zilio jiwa na Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, nao wakakhitalifiana kwacho na wakakitupa, basi jilazimishe kusimama sawa sawa wewe na Waumini walio pamoja nawe kuifuata Njia Iliyo Nyooka kama alivyo kuamrisha Mwenyezi Mungu. Wala msipindukie mipaka ya uadilifu kwa kupunguza, na kupuuza, na kuzidisha, kwa kuzikalifisha nafsi zenu kwa msilo liweza. Hakika Yeye Subhanahu ameyazunguka kwa ujuzi wake yote mnayo yatenda, na atakulipeni kwayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi kuwa na msimamo, ewe Nabii, kama alivyokuamrisha Mola wako, wewe na waliotubia pamoja nawe, wala msikipite kile Alichowaekea mpaka Allah Mtukufu. Hakika Mola wenu, kwa matendo yote mnayoyafanya, ni Muoni, hakuna kitu kinachofichika Kwake, na Atawalipa nyinyi kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net