Hud 11:111
هودوَإِنَّ كُلًّا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَـٰلَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ بِمَا يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ
Na hakika Mola wako Mlezi atawatimizia malipo ya matendo yao wote. Hakika Yeye anayo habari ya yale wanayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika Mola wako Mlezi atawatimilizia malipo ya vitendo vyao. Hakika Yeye anayo khabari ya wayatendayo. [111]
[111] Hapana shaka yoyote kila kikundi katika hawa Mola wako Mlezi atawalipa jaza ya vitendo vyao. Hakika Yeye Subhanahu ni Mjuzi wa ukamilifu wa kubwa na dogo wanayo yatenda, ikiwa kheri na ikiwa shari. Na atamlipa kila mmoja wapo kwa mujibu alivyo tenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakika watu wote hao wanaotafautiana tuliokutajia habari zao, ewe Mtume, Allah Mtukufu Atawatekelezea malipo ya matendo yao Siku ya Kiyama, yakiwa mema watalipwa wema na yakiwa maovu watalipwa uovu. Hakika Mola wako, kwa wanayoyafanya hawa washirikina, ni Mtambuzi, hakuna kitendo chao chochote kinachofichamana Kwake. Katika hii pana kitisho na onyo kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net