Hud 11:110
هودوَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ فَٱخْتُلِفَ فِيهِ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِىَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِى شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ
Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini kukazuka kuhitilafiana ndani yake. Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayowahangaisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa yakini tulimpa Musa Kitabu; zikazuka khitilafu ndani yake. Na lau kuwa si neno lilio kwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingeli hukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayo wahangaisha. [110]
[110] Na Sisi tunakuhakikishia, ewe Nabii, kwamba tulimpa Musa Taurati. Na watu wake baada yake wakakhitalifiana katika tafsiri yake na maana yake, kwa kufuata pumbao lao na matamanio yao. Kila mmoja wao anataka kuielekeza ifuate matamanio yake. Wakafarikiana makundi mbali mbali. Wengi wao wakajitenga na Haki iliyo wajia. Na lau kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu haikutangulia kuwa itaakhirishwa adhabu yao mpaka Siku ya Kiyama, ingeli wateremkia katika hii dunia yao hukumu ya Mwenyezi Mungu wakateketezwa wapotovu na wakaokoka walio na haki, kama yalivyo washukia wengineo, walio jiwa na ujumbe wakakhitalifiana katika kuufahamu baadae, na wakaugeuza, hata ikawa ni uzito kuifahamu kweli. Na hawa walio irithi Taurati wanababaika hawaijui kweli iko wapi!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakika tulimpa Mûsã Kitabu, nacho ni Taurati, wakatafautiana watu wake juu yake: baadhi yao walikiamini na wengine walikikanusha, kama walivyofanya watu wako kuhusu Qur,ani. Na lau si neno lililotangulia kutoka kwa Mola wako la kutowaharakishia adhabu viumbe Wake, ingaliwashukia wao duniani kwao hukumu ya Allah Mtukufu ya kuwaangamiza wenye kukanusha na kuwaokoa Waumini. Na makafiri wa watu wako, miongoni mwa mayahudi na washirikina, ewe Mtume, wako kwenye shaka inayowatia wasiwasi juu ya hii Qur,ani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net