Hud 11:109
هودفَلَا تَكُ فِى مِرْيَةٍ مِّمَّا يَعْبُدُ هَـٰٓؤُلَآءِ ۚ مَا يَعْبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعْبُدُ ءَابَآؤُهُم مِّن قَبْلُ ۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ غَيْرَ مَنقُوصٍ
Basi usiwe katika shaka juu ya yale wanayoyaabudu hawa. Hawaabudu isipokuwa kama walivyoabudu baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimizia fungu lao bila ya kulipunguza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi usiwe na shaka juu ya wanayo yaabudu hao. Hawaabudu ila kama walivyo abudu baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa. [109]
[109] Ilivyo kuwa hali ya watu washirikina walio dhulumu katika dunia na akhera ni hiyo tuliyo kusimulia, ewe Nabii, basi usiwe na shaka yoyote juu ya mwisho wa hao katika kaumu yako wanao abudu masanamu pindi wakiendelea katika upotovu wao. Kwani hali yao ni hali ya baba zao walio watangulia, ambao khabari zao tumekusimulia. Wote hao ni washirikina. Na Sisi tutawatimizia kwa ukafiri wao adhabu kaamili kwa kadiri ya makosa yao. Hawatapunguziwa hata chembe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi usiwe, ewe Mtume, katika shaka kuhusu ubatilifu wa vitu wanavyoviabudu washirikina hawa miongoni mwa watu wako. Wao hawaabudu, miongoni mwa masanamu, isipokuwa kama vile baba zao walikuwa wakiabudu huko nyuma. Na sisi ni wenye kuwatekelezea kile tulichowaahidi kikiwa kikamilifu kisichopunguzwa. Huu ni muelekezo kwa ummah wote, ingawa tamko lake limeelekezwa kwa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani ziwashukie).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net