Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 108

Hud 11:108

هود

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ سُعِدُوا۟ فَفِى ٱلْجَنَّةِ خَـٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَـٰوَٰتُ وَٱلْأَرْضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَ ۖ عَطَآءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ

Maana

Na ama wale waliofurahishwa, wao watakuwa katika Bustani wadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisicho na kikomo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ama wale walio bahatika, wao watakuwamo Peponi wakidumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisio na ukomo. [108]

[108] Ama wale ambao Mwenyezi Mungu amewajaalia kuwa na bahati njema wataingia Peponi wadumu humo tangu mwanzo, mara baada ya kwisha hisabiwa. Huko hakuna mwisho. Isipo kuwa kikundi ambacho Mwenyezi Mungu anataka kukiakhirisha kisiingie pamoja na wale wa mwanzo - na hao ni wale Waumini walio fanya maasi. Hao watacheleweshwa Motoni kwa kadiri ya kupata adabu ya kuwasafisha wapate kuingia Peponi. Na Mwenyezi Mungu atawalipa hawa walio bahatika malipo bora kabisa ya kudumu, yasio na kasoro, wala yasio katika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ama wale ambao Allah Mtukufu Amewaruzuku wema, wataingia Peponi wakae milele humo muda wa kuwako mbingu na ardhi, isipokuwa lile kundi ambalo Allah Mtukufu Atataka kulichelewesha, nalo ni lile la waliompwekesha Allah Mtukufu waliofanya maasia. Wao watasalia Motoni kwa kipindi fulani, kisha watatoka humo kwenda Peponi kwa matakwa ya Allah Mtukufu na rehema Yake. Na Allah Mtukufu Atawapa watu wema hawa vipaji visivyopunguzwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net