Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 107

Hud 11:107

هود

خَـٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَـٰوَٰتُ وَٱلْأَرْضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ

Maana

Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipokuwa atakavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda atakavyo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda apendavyo. [107]

[107] Watadumu Motoni muda wa kudumu mbingu na ardhi. Hawatotoka humo mpaka apendapo Mwenyezi Mungu, awaadhibu kwa adhabu namna nyengine! Ewe Nabii, Mwenyezi Mungu hutenda atakalo; hapana yeyote wa kumzuia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watakuwa ni wenye kukaa humo milele muda wa kuweko mbingu na ardhi, hivyo basi adhabu yao haitakatika wala haitakoma, bali ni adhabu ya daima iliyotiliwa mkazo, isipokuwa iwapo Mola wako atataka, kwa kuwatoa waliompwekesha waliofanya maasia baada ya muda fulani wa kukaa kwao Motoni. Hakika Mola wako ni Mwenye kufanya Analolitaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net