Hud 11:106
هودفَأَمَّا ٱلَّذِينَ شَقُوا۟ فَفِى ٱلنَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ
Ama wale waliojitia mashakani, hao watakuwa Motoni, humo watavuta pumzi na kuitoa kwa ugumu mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ama wale wa mashakani hao watakuwamo Motoni wakiyayayatika na kukoroma. [106]
[106] Ama wale wenye mashaka mwisho wao ni Motoni. Kuvuta pumzi kwao kutakuwa ni kwa machungu makubwa, na mikoromo na kuyayatika, wanapo vuta pumzi na kutoa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ama wale waliokuwa waovu ulimwenguni kwa kuharibika akida yao na uovu wa vitendo vyao, basi Moto utakuwa ndio mahali pao pa kutulia; humo watakuwa na kutoa pumzi kutoka kwenye vifua kwa nguvu na kurudisha kwa shida, na sauti mbili hizo ni mbaya zaidi zilizopita kiasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net