Hud 11:105
هوديَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِۦ ۚ فَمِنْهُمْ شَقِىٌّ وَسَعِيدٌ
Siku hiyo itakapokuja, nafsi yoyote haitazungumza isipokuwa kwa idhini yake. Basi miongoni mwao kutakuwa na walio mashakani na wenye furaha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Siku hiyo itakapo fika, hatosema hata mtu mmoja ila kwa idhini yake Mwenyezi Mungu. Kati yao watakuwamo waliomo mashakani na wenye furaha. [105]
[105] Kikija kitisho chake mwanaadamu hatoweza kusema ila kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu. Kwani miongoni mwa watu wapo wenye mashaka, dhiki, wasio na bahati kwa kila namna ya shida watazo pata. Hao ndio makafiri. Na wengine wenye furaha, walio bahatika, kwa neema zinazo wangojea Akhera. Hao ndio Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Siku kitakapokuja Kiyama, hakuna nafsi itakayosema isipokuwa kwa idhini ya Mola Wake. Kati yao kuna shaqiyy (muovu) anayestahili adhabu na kuna sa‛îd (mwema) aliyefadhiliwa kwa kupewa starehe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net