Hud 11:104
هودوَمَا نُؤَخِّرُهُۥٓ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ
Na wala hatuiahirishi isipokuwa kwa muda unaohisabiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Sisi hatuiakhirishi ila kwa muda unao hisabiwa. [104]
[104] Wala Sisi hatuiakhirishi ila kwa muda mfupi tuliyo kwisha uwekea kiwango. Na ingawa kwa nadhari ya watu itaonekana iko mbali, kwa Mwenyezi Mungu ni muda mchache tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatuicheleweshi Siku ya Kiyama isipokuwa ni ukome muda uliyohesabiwa uliyo kwenye elimu yetu, hauzidi wala haupungui na kipimo chetu tulichoupimia kwa hekima yetu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net