Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 101

Hud 11:101

هود

وَمَا ظَلَمْنَـٰهُمْ وَلَـٰكِن ظَلَمُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ ۖ فَمَآ أَغْنَتْ عَنْهُمْ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِى يَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ لَّمَّا جَآءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ

Maana

Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe walizidhulumu nafsi zao. Na miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipokuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia isipokuwa maangamio tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe wamejidhulumu. Na miungu yao waliyo kuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipo kuja amri ya Mola wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia ila maangamizo tu. [101]

[101] Wala Sisi hatukuwadhulumu kwa vile tulivyo wateketeza; lakini wamejidhulumu wenyewe kwa kufuru zao, na kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, na kuleta uharibifu katika nchi. Kwa hivyo miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu haikuweza kuwakinga na hilaki, wala haikuwafaa kitu ilipo kuja amri ya Mola wako Mlezi, ewe Nabii! Na kushikilia kwao kuabudu masanamu hakukuwazidishia ila hilaki na upotovu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakukuwa kuwaangamiza wao ni bila ya sababu na dhambi zinazowafanya wastahili hayo, lakini walijidhulumu wenyewe kwa ushirikina wao na kuleta kwao uharibifu katika ardhi. Hawakuwapa nafuu wao hao waungu wao ambao walikuwa wakidai kuwa ni waungu na wakiwataka wawaondolee shida, wakati amri ya Allah Mtukufu ilipokuja ya kuwaadhibu wao. Na hao waungu wao hawakuwazidishia isipokuwa uvunjaji, maangamivu na hasara.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net