Hud 11:102
هودوَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَآ أَخَذَ ٱلْقُرَىٰ وَهِىَ ظَـٰلِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُۥٓ أَلِيمٌ شَدِيدٌ
Na hivyo ndivyo ulivyo mshiko wa Mola wako Mlezi anapoishika miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mshiko wake ni mchungu na mkali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ndio kama hivyo ndivyo inavyo kuwa Mola wako Mlezi anapo ikamata miji inapo kuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali. [102]
[102] Na kuwateketeza kwa ukali kama huu, ewe Nabii, alivyo wateketeza Mola wako Mlezi kaumu ya Nuhu, na ya A'adi, na ya Thamud, na wengineo, ndivyo anavyo itwaa kwa nguvu miji inapo kuwa watu wake wanaingia katika dhulma kwa ukafiri na uharibifu! Hakika kuangamiza kwake Mwenyezi Mungu kuna nguvu, na kuna uchungu, na ukali kwa wenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kama nilivyowapatiliza kwa adhabu watu wa miji iliyodhulumu kwa kuenda kinyume na amri yangu na kuwakanusha Mitume wangu, nitawapatiliza wengineo miongoni mwa watu wa miji wakizidhulumu nafsi zao kwa kumkanusha Allah Mtukufu na kumuasi Yeye na kuwakanusha Mitume Wake. Hakika mapatilizo Yake ya mateso ni makali, yenye kuumiza, yaliyo magumu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net