Hud 11:100
هودذَٰلِكَ مِنْ أَنۢبَآءِ ٱلْقُرَىٰ نَقُصُّهُۥ عَلَيْكَ ۖ مِنْهَا قَآئِمٌ وَحَصِيدٌ
Hizi ni katika habari za miji, tunakusimulia. Mingine ipo bado na mingine ilifyekwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hizi ni katika khabari za miji, tunakusimulia. Mingine ipo bado na mingine imefyekwa. [100]
[100] Hadithi hio, ewe Nabii, ni baadhi ya khabari za miji tuliyo iteketeza. Tunakusimulia wewe upate kuwatolea mawaidha kwa khabari hizo watu wako, na utumaini kuwa Mwenyezi Mungu atakunusuru. Baadhi ya miji hiyo imekuwa kama mimea iliyo simama juu ya mashina yake ili waone yaliyo tokea, na baadhi yao imefutika athari yake kama mazao yaliyo kwisha vunwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haya tuliyokutajia wewe, ewe Mtume, ni miongoni mwa habari za watu wa miji ambayo tuliwaangamiza watu wake, twakupasha habari zake. Na miongoni mwa miji hiyo kuna iliyo na athari zilizosalia; na miongoni mwazo kuna ambazo athari zake zimefutika, hakuna chochote katika hizo kilichosalia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net