Hud 11:99
هودوَأُتْبِعُوا۟ فِى هَـٰذِهِۦ لَعْنَةً وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۚ بِئْسَ ٱلرِّفْدُ ٱلْمَرْفُودُ
Nao walifuatishwa laana hapa (duniani) na Siku ya Kiyama. Ni kipawa kibaya zaidi kilichoje walichopewa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nao wamefuatishiwa laana hapa duniani na Siku ya Kiyama. Ni mabaya yalioje watakayo pewa! [99]
[99] Na wao katika dunia hii iliwafuata laana ya Mwenyezi Mungu, na ya Malaika, na ya watu. Na Siku ya Kiyama kadhaalika itawafuata laana hiyo vile vile, kwani hiyo ndiyo zawadi yao. Zawadi hiyo ni ovu ya kuonyesha dhambi. Itasemwa : Ovu mno zawadi hii wapewao watu hawa!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Amewafuatishia laana katika ulimwengu huu, pamoja na adhabu Aliyowaharakishia ya kuzamishwa baharini. Na Siku ya Kiyama pia atawapa laana nyingine kwa kuwatia Motoni. Ni mabaya sana mambo yaliyokusanyika kwao na yakafuatana juu yao, ya adhabu ya Allah Mtukufu na laana ya duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net