Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 99

Yunus 10:99

يونس

وَلَوْ شَآءَ رَبُّكَ لَـَٔامَنَ مَن فِى ٱلْأَرْضِ كُلُّهُمْ جَمِيعًا ۚ أَفَأَنتَ تُكْرِهُ ٱلنَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ

Maana

Na angelitaka Mola wako Mlezi, wangeliamini walio katika ardhi wote kwa pamoja. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini? [99]

[99] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka watu wote katika ardhi waamini, wangeli amini. Basi wewe usihuzunike kwa ukafiri wa washirikina. Wala haiwi Imani ila kwa khiari. Basi wewe huwezi kuwalazimisha watu kwa nguvu ili wafuate Haki na waitikie. Haikupasii kutaka kuwalazimisha waamini, wala hutoweza, hata ukijitahidi vipi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau Mola wako, ewe Mtume, angetaka, watu wa duniani wote wangaliyaamini, kwa umoja wao, yale uliyokuja nayo, lakini Yeye ana hekima katika hilo. Yeye Anamuongoza Anayemtaka na Anampoteza Anayemtaka, kulingana na hekima Yake, na haliko kwenye uwezo wako jambo la kuwatendesha nguvu watu juu ya kuamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net