Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 98

Yunus 10:98

يونس

فَلَوْلَا كَانَتْ قَرْيَةٌ ءَامَنَتْ فَنَفَعَهَآ إِيمَـٰنُهَآ إِلَّا قَوْمَ يُونُسَ لَمَّآ ءَامَنُوا۟ كَشَفْنَا عَنْهُمْ عَذَابَ ٱلْخِزْىِ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَمَتَّعْنَـٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍ

Maana

Basi kwa nini haukuwepo mji ulioamini, kwa hivyo Imani yake ikaufaa, isipokuwa kaumu ya Yunus? Walipoamini, tukawaondolea adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia, na tukawastarehesha kwa muda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa nini usiwepo mji mmoja ukaamini na Imani yake ikawafaa - isipo kuwa kaumu Yunus? Waliamini na Sisi tukawaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia, na tukawastarehesha kwa muda. [98]

[98] Lau kila mji ungeli amini ingeli wafaa Imani yao. Lakini hawaamini, na kwa hivyo hayapatikani manufaa. Ila kaumu ya Yunus. Kwani wao waliamini, na wakapata manufaa yao. Tuliwaondolea hizaya na machungu, na tukawapa starehe ya dunia inayo pita, mpaka ifike Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Imani haikuwafaa watu wa mji wowote walioamini walipoishuhudia adhabu isipokuwa watu wa mji wa Yûnus mwana wa Mattã. Kwani wao walipohakikisha kwamba adhabu ni yenye kuwashukia, walirejea kwa Allah Mtukufu kwa kutubia kidhati; na ulipofunuka ukweli wa toba yao, Allah Mtukufu aliwaondolea adhabu ya hizaya baada ya kuwa karibu na wao, na Akawaacha ulimwenguni wakistarehe mpaka muda wao wa kuishi kukoma.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net