Yunus 10:100
يونسوَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تُؤْمِنَ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ وَيَجْعَلُ ٱلرِّجْسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ
Na haiwi kwa nafsi kuamini isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu juu ya wale wasiotumia akili zao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hawezi mtu kuamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu iwafike wasio tumia akili zao. [100]
[100] Hawezi mtu kuamini ila akiielekeza nafsi yake kwa hayo, na Mwenyezi Mungu akamsahilishia sababu na njia za hayo. Ama yule asiye ielekea Imani huyo basi amestahiki kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu, na kupata adhabu yake. Na mwendo wa Mwenyezi Mungu ni kuwapa adhabu na ghadhabu wale wanao zipuuza na kuzikataa hoja zilio wazi, na wala hawazizingatii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haikuwa nafsi yoyote ni yenye kumuamini Allah Mtukufu isipokuwa kwa idhini Yake na taufiki Yake. Basi usiisumbue nafsi yako katika hilo, kwani mambo yao yako kwa Allah Mtukufu. Na Allah Mtukufu Atajaalia adhabu na hizaya kwa wale ambao hawayatii akilini maamrisho Yake na makatazo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net