Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 101

Yunus 10:101

يونس

قُلِ ٱنظُرُوا۟ مَاذَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَمَا تُغْنِى ٱلْـَٔايَـٰتُ وَٱلنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ

Maana

Sema: Angalieni yaliyo katika mbingu na ardhi! Na Ishara zote na maonyo haviwafai kitu kaumu wasioamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Angalieni yaliomo mbinguni na kwenye ardhi! Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasio amini. [101]

[101] Ewe Nabii! Waambie hawa wenye inda: Tazameni Ishara zilizo wazi zinazo onyesha Ungu na Upweke wa Mwenyezi Mungu zilio enea katika mbingu na ardhi. Lakini Ishara, juu ya wingi wake, na maonyo na yangawa na nguvu, hayawafai kitu watu wanao kataa na wala hawatumii akili zao. Hawa wanao kanya kama hawaamini, basi hawatoangalia. Aya hii na Aya nyingi nyenginezo zinaita watu wajifunze kwa kuangalia na kuzingatia (Observation). Na inaita watu wajifunze ilimu ya ulimwengu na viliomo ndani yake, kwani huo ulimwengu umedhalilishwa kwa ajili ya mwanaadamu. Kisha hizo Aya zinataka watu waingie katika ilimu za kujaribu (Experimental Science). Kwani hiyo ni njia ya kujua kwa kuona vinavyo onekana.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu wako, «Fikirini na mzingatie kwa yaliyomo mbinguni na ardhini miongoni mwa aya za Allah Mtukufu zilizo waziwazi.» Lakini aya, mazingatio na Mitume wenye kuwaonya waja wa Allah Mtukufu adhabu Yake, vyote hivyo havikuwa ni vyenye kuwanufaisha watu wasioamini chochote katika hivyo, kwa sababu ya kupa mgongo kwao na ujeuri wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net