Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 102

Yunus 10:102

يونس

فَهَلْ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثْلَ أَيَّامِ ٱلَّذِينَ خَلَوْا۟ مِن قَبْلِهِمْ ۚ قُلْ فَٱنتَظِرُوٓا۟ إِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُنتَظِرِينَ

Maana

Basi, je, wanangojea kingine isipokuwa kama yale yaliyotokea siku za watu waliopita kabla yao? Sema: Ngojeni! Nami hakika ni pamoja nanyi katika wanaongoja.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi, je! Wanangojea jingine ila kama yaliyo tokea siku za watu walio pita kabla yao? Ngojeni! Nami ni pamoja nanyi katika wanao ngoja. [102]

[102] Basi hao wakanyao wanangojea lolote ila kufikiwa na siku za shida kama zilizo wapata kaumu ya Nuhu, na kaumu ya Musa, na wengineo? Ewe Nabii! Waambie: Ikiwa mnangojea mfano wa hayo, basi ngojeni! Nami pia nangojea pamoja nanyi. Na karibu hivi mtasibiwa na kushindwa, na Siku ya Kiyama mtapata adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawa hawangojei isipokuwa hiyo siku watakapoishuhudia adhabu ya Allah Mtukufu mfano wa siku za wakale wao waliokanusha waliopita kabla yao, Sema, ewe Mtume, «Ingojeeni adhabu ya Allah Mtukufu; hakika mimi ni mwenye kuingojea pamoja na nyinyi kuteswa kwenu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net