Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 103

Yunus 10:103

يونس

ثُمَّ نُنَجِّى رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na wale walioamini. Ndiyo kama hivyo, inatustahiki kuwaokoa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na walio amini. Ndio kama hivyo,inatustahiki kuwaokoa Waumini. [103]

[103] Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na Waumini kutokana na adhabu hiyo. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewaahidi kuwaokoa, na ahadi yake ni ya kweli, wala hayendi kinyume.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tutawaokoa Mitume wetu na wale walioamini pamoja na wao. Na kama tulivyowaokoa hao tutakuokoa wewe, ewe Mtume, na waliokuamini wewe kwa wema utokao kwetu na rehema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net