Yunus 10:90
يونسوَجَـٰوَزْنَا بِبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱلْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُۥ بَغْيًا وَعَدْوًا ۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَدْرَكَهُ ٱلْغَرَقُ قَالَ ءَامَنتُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱلَّذِىٓ ءَامَنَتْ بِهِۦ بَنُوٓا۟ إِسْرَٰٓءِيلَ وَأَنَا۠ مِنَ ٱلْمُسْلِمِينَ
Tukawavusha bahari Wana wa Israili, naye Firauni na askari wake wakawafuata kwa dhuluma na uadui. Mpaka kuzama kulipomfikia, akasema: Nimeamini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule ambaye walimwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea! [90]
[90] Tulipo wavusha bahari Wana wa Israili, Firauni na askari wake waliwafuatia nyuma yao, tukawafunika kwa bahari! Alipo kuwa anazama, Firauni alisema: Nimemsadiki Allah, Mwenyezi Mungu, walio msadiki Wana wa Israili, na wakamfuata. Na mimi ni katika wenye kut'ii walio wanyenyekevu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwakatia bahari Wana wa Isrãîl mpaka wakaivuka, wakafuatwa na Fir‛awn na askari wake, kwa udhalimu na uadui, wakafuata njia ya bahari nyuma yao, mpaka Fir‛awn alipozungukwa na hali ya kuzama alisema kwamba hapana Mola isipokuwa yule ambaye Wana wa Isrãîl wamemuamini, na mimi ni miongoni mwa wenye kumpwekesha Allah Mtukufu wenye kujisalimisha Kwake kwa kufuata na kutii.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net