Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 91

Yunus 10:91

يونس

ءَآلْـَٔـٰنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَ ٱلْمُفْسِدِينَ

Maana

Je, sasa? Na ilhali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa waharibifu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ala! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa mafisadi! [91]

[91] Mwenyezi Mungu hakukupokea kuamini huko kwa Firauni ambako alikuwa hana budi nako. Toba hiyo ilikuwa pale mauti yamekwisha mkabili, naye aliishi maisha yake yote katika kumuasi Mwenyezi Mungu, akifisidi nchi, naye akafa kafiri wa kutupwa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, sasa hivi, ewe Fir‛awn, wakati kifo kimekushukia ndipo unakubali kuwa wewe ni mja wa Allah Mtukufu na hali ulimuasi na ukawa ni miongoni mwa waharibifu wenye kuzuia njia Yake kabla ya adhabu Yake kukushukia! Basi toba haitokunufaisha wakati wa kukata roho na kushuhudia kifo na adhabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net