Yunus 10:89
يونسقَالَ قَدْ أُجِيبَت دَّعْوَتُكُمَا فَٱسْتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَآنِّ سَبِيلَ ٱلَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ
Mwenyezi Mungu akasema: Hakika maombi yenu wawili yameshakubaliwa. Basi nyookeni, wala msifuate njia ya wale wasiojua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu akasema: Maombi yenu yamekubaliwa. Basi simameni sawa sawa, wala msifuate njia za wale wasio jua. [89]
[89] Mwenyezi Mungu akasema: Dua zenu zimeitikiwa. Basi endeleeni katika Njia Iliyo Nyooka, na iwacheni njia ya wale wasio jua mambo yalivyo, wala hawaifuati Haki iliyo wazi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Akasema Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kuwambia wao wawili, «Yameshakubaliwa maombi yenu juu ya Fir‛awn na kundi lake na mali zao,- Mûsã alikuwa akiomba, na Hãrûn akiitika maombi yake, ndipo ikafaa kuyanasibisha maombi kwa wao wawili.- basi jikiteni kwenye Dini yenu na muendelee kumlingania Fir‛awn na watu wake kwenye kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtii, na msifuate njia ya asiyejua ahadi yangu njema na onyo langu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net