Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 88

Yunus 10:88

يونس

وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَآ إِنَّكَ ءَاتَيْتَ فِرْعَوْنَ وَمَلَأَهُۥ زِينَةً وَأَمْوَٰلًا فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّوا۟ عَن سَبِيلِكَ ۖ رَبَّنَا ٱطْمِسْ عَلَىٰٓ أَمْوَٰلِهِمْ وَٱشْدُدْ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُوا۟ حَتَّىٰ يَرَوُا۟ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ

Maana

Na Musa akasema: Mola wetu Mlezi! Hakika wewe umempa Firauni na wakuu wake mapambo na mali katika uhai wa dunia. Hivyo wanapoteza watu kutoka kwa njia yako. Mola wetu Mlezi! Zifutilie mbali mali hizo na zifunge nyoyo zao, wasiamini mpaka waione adhabu chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Musa akasema: Mola wetu Mlezi! Hakika wewe umempa Firauni na wakuu wake mapambo na mali katika maisha ya dunia. Hivyo wanapoteza watu na Njia yako. Mola wetu Mlezi! Yafutilie mbali mali yao na zifunge nyoyo zao, wasiamini mpaka waione adhabu chungu. [88]

[88] Walivyo shikilia makafiri katika kumfanyia inda Musa, alimwomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: Ewe Mola Mlezi wangu! Hakika Wewe umempa Firauni na watukufu wake starehe za duniani, na mali, na wana, na utawala. Na matokeo ya neema hizi ni kupita kwao mipaka katika kupotea na kupoteza watu waache Njia ya Haki! Ewe Mwenyezi Mungu! Yafutilie mbali mali yao, na uwaache katika kiza cha nyoyo zao, wasijaaliwe kuipata Imani mpaka waione kwa macho adhabu iliyo chungu, ambayo ndiyo mwisho unao wangojea, ili wawe ni onyo kwa wengineo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Mûsã akasema, «Mola wetu, hakika wewe umempa Fir‛awn na viongozi wa watu wake pambo la vitu vya duniani wasikushukuru, na wamejisaidia kwa vitu hivyo katika kupotoa watu na njia Yako. Mola wetu, yageuze Mali yao wasifaidike nayo, na uzipige mhuri nyoyo zao zisipate kuikunjukia Imani, wasiamini mpaka waione adhabu kali iumizayo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net