Yunus 10:87
يونسوَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّءَا لِقَوْمِكُمَا بِمِصْرَ بُيُوتًا وَٱجْعَلُوا۟ بُيُوتَكُمْ قِبْلَةً وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Na tukamteremshia ufunuo (wahyi) Musa na ndugu yake kuwa: Watengenezeeni majumba kaumu yenu katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndimo mahali pa ibada, na mdumishe Swala, na wape habari njema Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukampelekea Musa na ndugu yake wahyi huu: Watengenezeeni majumba watu wenu katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndio mwahali mwa ibada, na mshike Swala, na wabashirie Waumini. [87]
[87] Tukawafunulia Musa na nduguye Haruni kuwapa amri wafanye nyumba za kukaa watu wao katika nchi ya Misri, na watu wa Imani wenye kufuata wito wa Mwenyezi Mungu wazielekee nyumba hizo, na wawe wanashika Swala kwa sura ya ukamilifu. Na Waumini wanabashiriwa kheri!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwapelekea wahyi Mûsã na Hãrûn kwamba watengenezeeni watu wenu katika Misri majumba yenye kuwa ni makao na mahali pa hifadhi pa kukimbilia, na myafanye majumba yenu kuwa ni mahali pa kuswali ndani yake mkiwa na uoga, na tekelezeni Swala za faradhi kwa nyakati zake. Na wape Waumini wenye kumtii Allah Mtukufu bishara njema ya nguvu ya ushindi na thawabu nyingi kutoka Kwake, kutakata ni Kwake na kutukuka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net