Yunus 10:86
يونسوَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلْكَـٰفِرِينَ
Na utuokoe kwa rehema yako kutokana na kaumu hawa makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na utuokoe kwa rehema yako na watu makafiri. [86]
[86] Wakamwomba Mola wao Mlezi wakisema: Kwa vile ulivyo tumiminia neema na rehema, na kwa wingi wa rehema yako unayo sifika nayo, tuokoe na hawa watu wanao kataa, wenye kudhulumu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Na utuokoe, kwa rehema yako, kutokana na watu makafiri, Fir‛awn na kundi lake.» Kwani wao walikuwa wakiwalazimisha kufanya kazi ngumu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net