Yunus 10:85
يونسفَقَالُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu. Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa majaribio na hawa kaumu madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu. Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu. [85]
[85] Waumini wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu peke yake. Kisha wakamwomba Mola wao Mlezi asiwatie katika mitihani na mateso ya makafiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watu wa Mûsã walisema kumwambia, «Tumemtegemea Allah Mtukufu Peke Yake Asiye na mshirika na tumemwachia Yeye mambo yetu. Ewe Mola wetu, usiwape ushindi juu yetu ikawa ni mtihani kwetu katika Dini yetu, au ikawa ni mtihani kwa makafiri kwa kupata ushindi wakasema: lau wao (wenye kumuamini Mûsã) wako kwenye haki hawangalishindwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net