Yunus 10:84
يونسوَقَالَ مُوسَىٰ يَـٰقَوْمِ إِن كُنتُمْ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوٓا۟ إِن كُنتُم مُّسْلِمِينَ
Na Musa alisema: Enyi kaumu yangu! Ikiwa nyinyi mmemwamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Musa alisema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu, basi mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu. [84]
[84] Ama Musa aliwaambia Waumini kwa kuwawasa na kuwashajiisha: Enyi watu wangu! Ikiwa Imani imekwisha ingia nyoyoni mwenu kwa kumsafishia niya Mwenyezi Mungu, basi msimwogope yeyote mwenginewe. Nanyi msalimishie Yeye mambo yenu yote, na mtegemeeni Yeye, na muwe na yakini mwishoe atakunusuruni, ikiwa nyinyi mmethibiti katika Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na akasema Mûsã, «Enyi watu wangu, mkimuamini Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, na mkafuata sheria Yake, kuweni na imani na Yeye na jisalimisheni kwa amri Yake. Na kwa Allah Mtukufu jitegemezeni iwapo nyinyi ni wenye kumdhalilikia kwa utiifu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net