Yunus 10:83
يونسفَمَآ ءَامَنَ لِمُوسَىٰٓ إِلَّا ذُرِّيَّةٌ مِّن قَوْمِهِۦ عَلَىٰ خَوْفٍ مِّن فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِمْ أَن يَفْتِنَهُمْ ۚ وَإِنَّ فِرْعَوْنَ لَعَالٍ فِى ٱلْأَرْضِ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلْمُسْرِفِينَ
Basi hawakumwamini Musa isipokuwa baadhi ya vijana kutoka kwa kaumu yake, kwa kumwogopa Firauni na wakuu wao wasiwatese. Kwani hakika Firauni alikuwa jeuri katika ardhi. Na kwa yakini alikuwa miongoni mwa waliopita kiasi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi hawakumuamini Musa isipo kuwa baadhi ya vijana vya kaumu yake, kwa kumwogopa Firauni na wakuu wao wasiwatese. Kwani hakika Firauni alikuwa jeuri katika nchi. Na kwa yakini alikuwa miongoni mwa walio pita kiasi. [83]
[83] Na juu ya kudhihiri Ishara zote za kusadikisha Ujumbe, wale walio muamini Musa hawakuwa ila ni kikundi cha watu wachache tu katika kaumu ya Firauni. Waliamini juu ya kuwa wakiogopa asije Firauni na walio pamoja naye wakawaachisha waliyo yaamini. Jeuri za Firauni zilikuwa kubwa mno katika Misri! Hakika yeye ni katika walio pita upeo katika kutakabari na kujivuna.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawakumuamini Mûsã, amani imshukie, pamoja na hoja na dalili alizowaletea, isipokuwa kizazi cha watu wake, Wana wa Isrãîl, hali ya kuwa wao wana uoga na Fir‛awn na kundi lake wasiwatese kwa kuwaadhibu na wasiwazuie na Dini yao. Na hakika Fir‛awn ni mjeuri mwenye kiburi katika ardhi, na hakika Yeye ni miongoni mwa waliopita mpaka katika ukafiri na uharibifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net