Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 82

Yunus 10:82

يونس

وَيُحِقُّ ٱللَّهُ ٱلْحَقَّ بِكَلِمَـٰتِهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْمُجْرِمُونَ

Maana

Na Mwenyezi Mungu huihakikisha haki kwa maneno yake, hata wakichukia wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu huhakikisha Haki kwa maneno yake, hata wanga chukia wakosefu [82]

[82] Ama Haki hapana shaka Mwenyezi Mungu atainusuru na ataiunga mkono kwa uwezo wake na hikima yake hata makafiri wakisaidiana katika kuichukia na kuipiga vita.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Atauimarisha ukweli niliokuja nao kutoka Kwake Ataufanya uwe juu ya ubatilifu wenu kwa maneno Yake na amri Yake, ingawa watu wahalifu wenye kufanya maasia, miongoni mwa jamaa za Fir‛awn, wanachukia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net